FR EN
KANUNI 107 ZA PESA : Jinsi ya kuzichuma na kuzitunza kusudi ujitegemee kipesa kwa muda mrefu
Shammy Bunani

KANUNI 107 ZA PESA : Jinsi ya kuzichuma na kuzitunza kusudi ujitegemee kipesa kwa muda mrefu

(0 reviews)
Author:Shammy Bunani
Language:SW
Pages:245
Format:PDF, Kindle, Paperback
$14.29 $16.07
Login to Purchase

About the Book

Kazi kubwa na ya kipekee ya Richard Templar, iliyotafsiriwa, kuboreshwa na kuhuishwa kwa umahiri mkubwa na Shammy Bunani (DRC) akishirikiana na Bertha Kapala (Tanzania).

Je, unajua siri ya mafanikio ya kifedha?

Pesa ina kanuni zake. Hata hivyo, vitabu vingi vya uchumi vinajaa nadharia ngumu na mambo ya kitaaluma yaliyopo mbali sana na maisha yako ya kila siku.

Kitabu hiki kiko tofauti kabisa. Kanuni 107 za Pesa si mwongozo wa mambo ya kufikirika; ni ramani ya vitendo, mkusanyiko wa misingi ya maisha na mikakati thabiti ya kuvunja ukuta wa umaskini na kufungua milango ya utajiri wa kudumu.

Kujitegemea kifedha si bahati au fursa kwa ajili ya watu wachache waliojaliwa; ni matokeo ya maamuzi sahihi na kufuata kwa nidhamu kanuni zilizothibitishwa. Iwe wewe ni mjasiriamali, mfanyakazi anayetafuta mwelekeo, au mtu yeyote mwenye nia ya dhati ya kubadilisha hatimiliki yake ya kiuchumi, kitabu hiki kina hazina unayoitafuta.

Mambo utakayojifunza katika kitabu hiki:

Kikiwa kimegawanywa katika sehemu kuu tano za kimkakati, mwongozo huu utakuongoza hatua kwa hatua kuelekea uhuru wa kifedha :

Sehemu ya Kwanza: Fikra za Kitajiri (Kuwa na Akili ya Pesa) – Amsha mtazamo wa kisaikolojia unaohitajika. Tambua na uvunje dhana potofu zinazorudisha nyuma juhudi zako za kujitafutia maendeleo.

Sehemu ya Pili: Kushika Pesa (Kutafuta Utajiri) – Chukua hatua ukiwa na mpango madhubuti. Jifunze sanaa ya kujadiliana, kuuza, kuthubutu kukabili riski, na kutumia chini ya kile unachokiingiza.

Sehemu ya Tatu: Kuzidisha Utajiri – Ifanye pesa ikufanyie kazi. Ongeza vyanzo vyako vya mapato, pata washauri (mentors) sahihi, na jifunze jinsi ya kukuza rasilimali zako.

Sehemu ya Nne: Kulinda Utajiri Wako – Kupata pesa kunahitaji kipaji, lakini kuzitunza kunahitaji nidhamu kubwa. Linda mtaji wako, weka akiba ya dharura, na ujue ni lini unapaswa kuridhika na kusimama.

Sehemu ya Tano: Kushiriki Utajiri Wako na Wengine – Gunduwa sanaa ya ukarimu na utumiaji wa busara wa utajiri wako ili kuleta athari chanya katika jamii na kwa watu wako wa karibu bila kutengeneza tegemezi.

Upekee wa toleo hili lililoboreshwa:

Hili si tu tafsiri ya lugha, bali ni kazi iliyoboreshwa kwa kuongezewa mifano halisi, mikakati ya kivitendo na maelezo ya kina yanayoendana kikamilifu na mazingira, changamoto, na fursa za kiuchumi za ukanda wetu. Kila kanuni imechambuliwa ili iwe rahisi kueleweka na kuanza kutumika mara moja.

« Pesa ni rasilimali ya mpito; lakini akili yako, afya yako, maadili yako na mahusiano yako ya dhati ndio chanzo pekee endelevu cha mafanikio yako. »

Acha kuwa mtazamaji wa mafanikio ya wengine. Zamia kwenye kanuni hizi 107, ziishi, na ugundue hazina inayokusubiri kwa ajili ya mustakabali wako wa kifedha!

______________________________

Des connaissances pour agir, des cles pour reussir

Shammy Bunani

Directeur.

Product Details

  • Publisher: Untresor Editions
  • Language: SW
  • Pages: 245
  • Publication Date: May 28, 2026

Customer Reviews

0
0 ratings

No reviews yet. Be the first to review this book!